• Yahusuyo

Kanisa la Kristo

~ "…makanisa ya Kristo yakusalimu," Warumi 16:16

Tag Archives: Imani

‘KUAMINI’ MAANA YAKE NINI?

01 Saturday Aug 2015

Posted by chimalaheath in Uncategorized

≈ Leave a comment

Tags

Imani, Wokovu

‘KUAMINI’ MAANA YAKE NINI?

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe nauzima wa milele” Yohana 3:16. Mstari huu ni moja ya mistari inayopendwa katika Biblia, na bado ni moja ya mistari ya Biblia iliyokosewa kueleweka. Sintofahamu hiyo hutokana na watu kuchanganya maana ya “kuamini”. Wengine hufundisha kuwa neno “amini” hapa humaanisha tu kumtambua Yesu kama mwokozi, na kwamba endapo wakifanya hivyo wanakuwa kwenye hali ya kuokolewa.

Neno “amini” katika Yohana 3:16 hutokana na neno la Kiyunani pisteuo, linalomaanisha ushawishi, tumaini la furaha, muunganiko wa utiifu. Neno “amini” katika Agano Jipya mara nyingi hubeba dhana ya utii. Neno hili pekee yake halimaanishi “saini ya kifikra.”

Mtu anaweza kutazama mazingira ambayo waziwazi Yohana 3:16 huangukia na ataweza kuona ushahidi kwamba katika mstari huu Yesu alimaanisha mambo mengi zaidi ya saini ya kifikra. Mazingira yenyewe ni Yohana 3:1-21. Na katika mistari hii twajifunza mambo matatu ambayo nataka kuyazingatia:

  1. Ili mtu awe ndani ya Yesu, ni lazima azaliwe mara ya pili, kuzaliwa kwa maji na kwa roho, Yohana 3:1-8.
  2. Katika Yohana 3:14 kuna nukuu ya Musa kumwinua nyoka jangwani. Hata kale, waliomtenda Mungu dhambi, hawakukaa tu nyumbani huku wakiamini kuwa yule nyoka wa shaba angewaokoa. Kimsingi walitakiwa kuinuka, kutembea kutoka hemani mwao, ambapo yawezekana ilikuwa ni umbali wa maili kadhaa (kumbuka kulikuwa na kambi ya watu wapatao milioni tatu) ili kufika mahali palipokuwa na yoka wa shaba ili kumtazama ili wawe hai, Hesabu 21:9. Ni wazi kwamba katika wokovu wao kulikuwa na zaidi ya saini ya kifikra

3) Yesu alidhihirisha kwamba endapo unataka kuijia nuru, kulikuwa na jambo ambalo mtu ulitakiwa kulifanya, “Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru,” Yohana 3:21.

Tuelewe kutokana na Neno la Mungu kuwa imani ya Kibiblia huhusisha imani inayompelekea mtu kutumaini na kutii. Kushindwa kutumaini na kumtii Yesu ni kushindwa dhahiri kumpokea kama Bwana na mwokozi. “Na kwanini mwaniita Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?” Luka 6:46

Masomo Mapya

  • Ala Za Muziki Katika Ibada
  • Ubatizo Wa Watoto
  • ‘KUAMINI’ MAANA YAKE NINI?
  • Kunyunyizia, Kumwagia, Au Kuzamisha – Ni Upi?
  • Biblia Yasema Nini…..Kuhusu Petro?

Brown Trail Church of Christ

1801 Brown Trail
Bedford, Texas, 76021
kanisalakristo@yahoo.com
Mpango Wa Wakovu

Kusikia - Rum 10:17
Kuamini - Yoh. 8:24
Kutubu - Luka 13:3, 5
Kukiri - Mat. 10:32; Mdo. 8:37
Kubatizwa - Mdo. 2:38

Blogroll

  • Brown Trail Church of Christ
  • Brown Trail School of Preaching
  • Graceton Church of Christ
  • Heath Stapleton
  • Kanisa la Baptist
  • Kanisa La Kiinjili La Kilutheri
  • Kanisa la Kristo
  • Mshahidi Wa Yehova
  • Robert Stapleton

Ingiza anwani yako ya barua pepe ili kuifuatilia blogu hii na utakuwa unajulishwa masomo mapya.

Join 3 other subscribers

Kwa Masomo Kwa Njia Ya Posta

Mbeya:

Kanisa la Kristo Kalobe
S.L.P. 2962
Mbeya, Tanzania
reachingtheperishingsouls@
gmail.com

Mwanza:

Kanisa la Kristo Buzuruga
S.L.P. 7568 Nyakato
Mwanzo, Tanzania
cskapala@gmail.com

Create a free website or blog at WordPress.com.

Privacy & Cookies: This site uses cookies. By continuing to use this website, you agree to their use.
To find out more, including how to control cookies, see here: Cookie Policy
  • Follow Following
    • Kanisa la Kristo
    • Already have a WordPress.com account? Log in now.
    • Kanisa la Kristo
    • Customize
    • Follow Following
    • Sign up
    • Log in
    • Report this content
    • View site in Reader
    • Manage subscriptions
    • Collapse this bar